The House of Favourite Newspapers

MABAO YOTE YA YANGA VS MBAO FC 2-0 (VIDEO)

MECHI ya Yanga na Mbao FC imemalizikakatika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku wenyeji Yanga wakizidi kujikusanyia pointi baada ya kufunga Mbao, mabao 2-0.

 

Bao la kwanza limepachikwa kimiani na Rafel Daud dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Ajibu bao lililodumu kwa kipindi chote cha kwanza cha mechi hiyo.

 

Kipindi cha pili Mbao walijitahada kuja kwa kasi kushambulia lango la Yanga lakini haikuweza kusaidia kitu. Licha ya mashambulizi hayo, Mbao FC walipata nafasi zingine kama nne kipindi cha kwanza lakini walishindwa kuzitumia vema.

 

Zikiwa zimeongezwa dakika tano, Ibrahim Ajibu alifanikiwa kuingia kambani kwa kufunga bonge la bao kwa tikitaka ya aina yake na kuifanya Yanga iwe mbele kwa mabao 2-0.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 2 na Mbao FC 0. Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 16 katika msimamo wa ligi huku Mbao ikisalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya 5.

Shuhudia Mabao Yote

Comments are closed.