The House of Favourite Newspapers

Magufuli afunika Kisarawe na Ukonga leo‏

0

magufuli akimwaga sera viwanja vya moshi bar ukonga (1)

magufuli akimwaga sera viwanja vya moshi bar ukonga (2)

Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa jimbo la Ukonga mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa Moshi Bara,Dkt Magufuli amemaliza mkutano wake wa kampeni jimbo la Kisarawe,Ukonga na  baadae anatarajia kuhutubia mkutano wa Kampeni Pemba na Unguja.

 

magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Jerry Slaa wakijadiliana jambo

Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Ukonga Jerry Slaa wakijadiliana jambo.

wakazi wa ukonga walivyompokea magufuli (3)

Wakazi wa Ukonga walivyompokea Magufuli kwa kupiga push up.

wakazi wa ukonga walivyompokea magufuli (2)

Wakazi wa Ukonga wakimshangilia Magufuli baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Moshi bar Ukonga.

wakazi wa kisarawe wakimsiliza maguyfuli alipokuwa akimwaga sera

wakazi wa Kisarawe wakimsiliza Magufuli alipokuwa akimwaga sera.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Pombe Magufuli baada ya mapumziko ya Nyerere day leo alianza kampeni kwa kishindo katika viwanja vya Bomani Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, baada ya mkutano huo Magufuli alipokelewa kwa hoihoi na vifijo kwenye jimbo la Ukonga ambapo alikwenda kufanya mkutano uliohudhuliwa na umati mkubwa wa watu kwenye viwanja vya Moshi bar jimboni Ukonga.

Katika mikutano hiyo Magufuli aliwaahidi wananchi hao kutatau mataizo mbalimbali likiwemo suala la kuweka lami kwenye maeneo hayo.

Magufuli  alisema atatengeneza barabara mpya kutoka Dar Chalinze mpaka Morogoro ambayo itakuwa na fly over saba. Leo saa saba mchana anatarajia kusaini mkataba mpya wa kuweka fly over pale makutano ya Tazara.

(Habari/Picha: Richard Bukos)

Leave A Reply