The House of Favourite Newspapers
gunners X

Magufuli Ateua Baraza la Mawaziri

0

magufuli

RAIS   John Magufuli, Desemba 5, 2020,  ameteua baraza la mawaziri ambapo orodha hiyo imesomwa   na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

 

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ni Elias Kwandikwa,  Wizara Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ni  Capt. Mst. George Mkuchika.

 

Wizara ya Ardhi ni William Lukuvi, Wizara ya Maji ni Juma Aweso, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  ni Innocent Bashungwa, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ni  Jenista Mhagama

 

Wizara ya Afya ni Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye pia rais amemtea kuwa Mbunge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji ni Prof. Kitila Mkumbo,  Wizara ya Katiba na Sheria -ni. Dkt. Mwigulu Nchemba  naWizara ya Elimu -niProf. Joyce Ndalichako.

 

Wizara ya Mifugo na Uvuvi ni Mashimba Mashauri Ndaki, Wizara ya Maliasili na Utalii ni Dkt. Ndumbaro Damas Daniel,  Ofisi ya Rais TAMISEMI ni. Selemani Jafo, Wizara ya Nishati ni Dkt. Medard Kalemani,  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ni Leonard Chamuriho na Wizara ya Kilimo ni  Prof. Adolf Mkenda.

 

Wizara ya Madini  ni Dkt. Doto Biteko, Wizara ya Viwanda na Biashara ni Geoffrey Mwambe, na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni George Simbachawene

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ni Ummy Mwalimu, Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (wizara mpya)  ni Dkt. Faustine Ndugulile.

Leave A Reply