The House of Favourite Newspapers

Magufuli Ampigia Chapuo Katambi Ubunge – Video

0

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  John Magufuli,  leo  Septemba 03, 2020, amewaomba wananchi wa Shinyanga kumpa kura mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika katika uwanja wa Kambarage.

 

Pamoja na hayo Magufuli ameelezea mipango ambayo anatarajia kuikamilisha katika Mkoa wa Shinyanga iwapo atarejea madarakani baada ya uchaguzi.

“Hapa Shinyanga tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, kwani tumepeleka umeme katika vijiji 136 vya mkoa huu,” alisema huku akiahidi kukamilisha pia miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo.

Leave A Reply