The House of Favourite Newspapers

Magufuli, Lowassa Wafunguka 2018

Rais Dk. John Magufuli.

RAIS Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, wamewatakia Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2018.

 

Katika salamu yake, Rais Magufuli aliwaomba Watanzania Watanzania kudumisha amani, upendo na mshikamano, sambamba na kufanyakazi kwa bidii ili kujenga nchi.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

“Ndugu zangu Watanzania, nawatakia heri ya mwaka mpya 2018, naungana nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa baraka zake, nawaomba tuendelee kudumisha amani, upendo, mshikamano wetu na tuchape kazi kwa juhudi na maarifa, kwa maendeleo ya Taifa letu ili tujenge Tanzania mpya,” alisema Rais Magufuli katika ujumbe wake alioandika kwenye ukurasa wa twitter.

 

LOWASSA

Kwa upande wake, Lowassa aliwataka Watanzania mwaka 2018 wakatae kugawanywa kwa namna yoyote ile.

Lowassa kupitia ukurasa wake wa twitter, aliwatakia Watanzania heri ya mwaka mpya wa 2018.

“Tunapouanza mwaka huu mpya niwaombe Watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile,“aliandika Lowassa.

Alisisitiza kuwa,“umoja na mshikamano ndio nguzo yetu. Nawatakia heri na fanaka ya mwaka mpya 2018.”

Comments are closed.