The House of Favourite Newspapers

Maguire Amsamehe Mbunge wa Jimbo la Bolgatanga Central, Nchini Ghana

0

BEKI wa Manchester United, Harry Maguire amemsamehe Mbunge wa Jimbo la Bolgatanga Central, Nchini Ghana, Isaac Adongo ambaye mwaka jana alifananisha hali mbaya ya uchumi wa Nchi hiyo na kiwango cha beki huyo.

Jana akiwa bungeni, Adongo amesema Maguire kwasasa sio yule wa zamani. “Mhe. Spika unakumbuka kwamba mwaka jana, nilikuwa mwepesi sana kumlinganisha kaka yangu mkubwa, Dkt Mahamudu Bawumia na Harry Maguire. Mhe. Spika, sasa naomba radhi kwa Harry Maguire. Leo Maguire amegeuka, ni mwanasoka wa mabadiliko” amesema.

“Harry Maguire sasa anafunga mabao Manchester United. Harry Maguire sasa ni mchezaji muhimu wa Manchester, kwani kwa Maguire wetu [Dk Bawumia], sasa anazurura huko IMF akiwa na kikombe mkononi. Kuhusu Maguire wetu wa kiuchumi, aliweza kuwafanya wastaafu wetu kuondoka majumbani mwao na kuja kufanya gwaride mitaani,” aliongeza Adongo.

Isaac Adongo anadai wakati akifanya tathmini hiyo, nyota huyo wa England na Mkuu wa Timu ya Usimamizi wa Uchumi Nchini Ghana hawakuwa wakitekeleza majukumu yao kulingana na matarajio ya watu.

Hata hivyo ameongeza kuwa Maguire amepindua meza kwa kubadilika wakati Dkt Bawumia akiiongoza nchi hiyo kwenye madeni.

Maguire sasa amekubali msamaha wa Adongo. Akijibu ukosoaji wa Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X (zamani Twitter), nahodha huyo wa zamani wa United ameandika: “Mbunge Issac Adongo nimepokea msamaha wako. Tuonane Old Trafford hivi karibuni.”

DANGOTE AZIKWA KIKACHERO NA WATU 7 USIKU MVUA IKINYESHA WAANDISHI WAGEUKA NDO WAZIKAJI HAKUNA PICHA

Leave A Reply