Maguire ataifanya United iwanie ubingwa

PEP Guardiola anaamini kwamba sasa Manchester United itaweza kupigania ubingwa wa Premier baada ya kumnasa beki, Harry Maguire kutoka Leicester City.

 

City na Liverpool waliziacha timu nyingine kwa tofauti ya pointi 25 kwenye msimamo wa Premier msimu uliopita lakini kocha huyo wa City anaamini kwamba safari hii wapinzani watakuwa wengi, hasa baada ya United kuipiku Man City kwenye dili la Maguire.

 

Alipoulizwa kama Maguire ni mtu sahihi wa kuirejesha United kwenye vita ya ubingwa, Guardiola alisema: “Ndiyo. Ni mchezaji bora, wa daraja la juu. “Tulikuwa tunamtaka lakini hatukuweza kummudu na United iliweza.

 

Ni bora sana kwa mipira ya juu, ni mzuri akiwa na mpira na anakimbia na mpira haraka.

 

“Sijui kama mbio za safari hii zitakuwa kama msimu uliopita; timu mbili pekee za kuwania ubingwa. Nadhani United wamenunua.

 

Arsenal pia na Tottenham pamoja na Chelsea. Kwa hiyo nadhani wapinzani watakuwa wengi msimu huu.” City bado wanasaka beki baada ya kuondoka kwa Vincent Kompany.

YANGA Wajibu Tuhuma Za SIMBA, Wafungukia MCHEZO Wa KESHO.


Loading...

Toa comment