The House of Favourite Newspapers

Mahusiano Birdman, Ton Braxton Nd’o ‘Bye Bye’

 

RAPA Birdman na aliyekuwa mchumba wake, Ton Braxton, mahusiano yao yamefikia tamati mwishoni mwa mwaka 2019 na mwanzoni mwa 2019.

 

Siku ya mwaka mpya tarehe moja, rapa huyo aliweka video kwenye instagram stori iliyokuwa inasomeka, “imekwisha” na baada ya muda alifuta kila kitu kwenye akaunti yake.

 

Kwa upande wake, Braxton alifuta post zote katika akaunti yake na kuweka post aliyovaa nguo nyekundu huku ikiambatana na maelezo yaliyosomeka, “Kuanza ukurasa mpya si chaguo rahisi, lakini kila wakati chagua kuchaguliwa” akamalizia na kuwatakia mashabiki mwaka mwema.

 

Wawili hao wamekuwa marafiki kwa muda wa takribani miaka 17, mahusiano yao yalianza 2016 na mwaka 2018 walitangaza uchumba.

Comments are closed.