Coachella Yatangaza Orodha ya Watumbuizaji Mwaka 2019

 

TAMASHA kubwa la muziki duniani ambalo hufanyika kila mwaka nchini Marekani la ‘Coachella’, jana waandaji wake wametangaza orodha ya majina kibao ya wasanii na MaDJ watakaotumbuiza.

 

Kwenye orodha hiyo kuna majina mawili ya wasanii kutoka Afrika ambao ni Burna Boy na Mr Eazi kutoka Nigeria. Mwaka jana kwenye tamasha hilo Afrika iliwakilishwa na Wizkid na Black Coffee kutoka Afrika Kusini.

 

Mafanikio ya mwaka jana ya mwanadada Ella Mai yamemwezesha kupata nafasi ya kutumbuiza katika orodha ya kwanza. Wasanii wengine wakubwa watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni  Ariana Grande, Childish Gambino, Wiz Khalifa na J Balvin.

 

Tamasha hilo linategemewa kufanyika kuanzia 12 Aprili hadi April 14, 2019 huko California.

 

Toa comment