The House of Favourite Newspapers

MAI: KWA BUTI LA ZARI, WABONGO TUMEKAA!

Maimartha Jesse ‘Mai’

GHARAMA ya kiatu ‘buti’ alichokuwa amevaa mwanamama Zarina Hassan ‘Zari’ kwenye picha zake mpya Instagram, limemshitua Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ na kukiri kuwa, atakuwa amewakalisha Wabongo wengi.

 

Buti hilo ambalo ni brandi ya Kanye West linalotajwa kugharimu dola 645 za Kimarekani (takribani shilingi milioni 1.5) wamekuwa wakionekana wamelivaa mastaa wakubwa duniani kama Rihanna na Kim Kardashian hivyo kuvaliwa na Zari kumewashtua wengi.

Akizungumza na gazeti hili, Maimartha alisema: “Zari si mwanamke wa mchezo mchezo, kwa hili buti lake amewakalisha wengi, mara nyingi akiweka mavazi na bei zake watu husema ni feki lakini kwa kiatu hiki naamini bei yake ni ya ukweli.” Zari mara nyingi hujipenda na kila akivaa vazi jipya hutupia na bei ya vazi hilo lakini historia imekuwa ikionesha kuwa, mara nyingi watu hasa Wabongo humbeza na kueleza kuwa huweka bei feki.

STORI: Mwandishi Wetu, Dar

Comments are closed.