The House of Favourite Newspapers

Mai: Soko la Filamu Halijashuka

0

Mai (2)

Maimuna Salum  maarufu kwa jina la “Mai Vituko Show”.

Na Leonard Msigwa

DAR ES SAALAM: Mwanadada anayechipukia kwa kasi kwenye soko la filamu na michezo ya kuigiza kwenye runinga Bongo, Maimuna Salum (18), maarufu kwa jina la “Mai Vituko Show” amefunguka na kupinga vikali wanaosema soko la filamu Bongo limeshuka na halilipi.

Mwanadada huyo ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye kituo cha runinga cha Channel Ten amesema hayo alipozungumza na Global Digital na kusema:

“Sikubaliani na wanaosema soko la filamu Bongo limeshuka, mimi naona wanaosema hivyo wameishiwa ubunifu na ujuzi wa namna bora ya kuandaa filamu zao kulingana na wakati uliopo, bado naamini kama ukiwa mbunifu na ukitengeneza kitu cha tofauti lazima utaona filamu ni ajira na inalipa, jambo la muhimu wasanii tuache kuigana, tuboreshe zaidi.”

Mai (1)-001

Mai Vituko Show.

Alipoulizwa changamoto gani anazokutana nazo kama msanii chipukizi amesema:

“Changamoto zinatofautiana ila kwangu kubwa ni baadhi ya waongoza filamu kunitaka kimapenzi na kuna mmoja aliwahi kugoma kunipa nafasi mpaka nimpe penzi, nikaamua kuacha kazi na kuja kuomba huku Vituko Show ambako mambo kama hayo sijayaona.

“Namwomba Waziri Nape Nnauye atusaidie vijana wenye ndoto ya kuwa waigizaji wakubwa tuweze kufikia malengo yetu kwa serikali au wizara iliyo chini yake kuweka njia bora na wazi kutuwezesha vijana.”

Leave A Reply