The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Maimamu Watoa Tamko Mauaji ya Imamu Msaidizi

0

MAIMAMU wa msikiti wa Al-Kheri uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam, wametoa tamko la kuliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuunda Tume itakayowahusisha viongozi na wataalamu kuchunguza vifo mbalimbali vilivyotokea katika mazingira ya kutatanisha.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar, Imamu Amiri Yusuf Salum amesema kuwa mauaji ya hivi karibuni ya kijana Salum Almasi aliyekuwa Imam Msaidizi wa Msikiti wa Kurasini yamejaa utata, kwani ndugu na muonekano wa marehemu unakinzana na maelezo ya Polisi.

“Taswira ya picha ya marehemu haiashirii kama alikuwa anataka kupora fedha kwani alikuwa amevalia kofia yake kichwani hali ambayo haionyeshi mtu aliyekuwa akipambana kwa judo,” alisema.

Katika tamko lao wamesema kuwa kumekuwa na utamaduni kwa Jeshi la Polisi kuhusisha aya za Qur’ani tukufu na matendo ya ujambazi au ugaidi kwamba askari hudai kuwa wahalifu wanapokwenda kufanya uhalifu ndio hufanya hayo.

Marehemu Salum pia alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliuawa na Polisi Kurasini karibu na Makao Makuu ya Uhamiaji kwenye ATM ya CRDB.

NA DENIS MTIMA|GPL

Leave A Reply