The House of Favourite Newspapers

MAIMARTHA AMKINGIA KIFUA WEMA

Maimartha Jesse ‘Mai’

BAADA ya kuwa na mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nani anayependwa na kukubalika zaidi Tanzania kati ya mwanamitindo, Hamisa Mobeto na Wema Isaac Sepetu, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse ‘Mai’ ameliamsha dude na kuonesha upande wake.  Akipiga stori na Za Motomoto News, Mai alisema hakuna na hatatokea mrembo mwingine anayependwa na kukubalika kama Wema hivyo wanaompigia debe Mobeto kwamba ndiye anayekubalika sana kwa sasa wanajisumbua tu.

“Wema ndiye Tanzania Sweetheart, hakuna wa kufanana naye na hatatokea mwingine kama yeye, hii ni namba nyingine, wanaosema Mobeto anamzidi ni waongo na hawajafanya tathmini zao vizuri, Wema anapendwa na kila mtu kuanzia watoto hadi wazee,” alisema Mai.

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.