MAITI YA TSHISEKEDI KUREJESHWA DRC BAADA YA MIAKA MIWILI

MWILI wa aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Étienne Tshisekedi, utarejeshwa nyumbani Mei 30 na kuzikwa Juni 1, mwaka huu.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya familia Tshisekedi, mwili huo utarejeshwa nchini humo baada ya miaka miwili kupita tangu alipofariki dunia akiwa mjini Brussels nchini Ubelgiji mwezi Februari 1, 2017.

Baada ya kifo chake kulizuka utata ni wapi angezikwa kwani uongozi wa chama chake cha UDPS, ulitaka azikwe kwenye makao makuu ya chama hicho katikati ya Jiji la Kinshasa, lakini serikali wakati huo ikiongozwa na rais Joseph Kabila ikakataa.

 

Tshisekedi ambaye alikuwa ni baba wa rais wa sasa na taifa hilo, Felix Tshisekedi, aliwahi kuwania urais mara kadhaa nchini humo na alikuwa ni mpinzani wa  Kabila Kabange.

Alizaliwa Desemba 14, 1932.

 

Loading...

Toa comment