The House of Favourite Newspapers

MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI YA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Shibuda,(kushoto) katika kikao kati yake na kamati hiyo, ofisini kwake Jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa nchini, Ofisini kwake Jijini Dodoma, Aprili 27, 2018. Kulia kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu), Maimuna Tarishi na kushoto kwake ni  Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John  Shibuda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwasababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.

 

Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.

 

Ameyasema hayo leo Ijumaa, Aprili 27, 2018 wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa waziri mkuu ulioko Mlimwa Jijini Dodoma.

 

“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujiletea maendeleo.”

 

Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

 

Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.

 

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

L. P. 980,

DODOMA.

 

Comments are closed.