The House of Favourite Newspapers

Majambazi wateka kijiji kwa saa 3, wajeruhi na kupora fedha!

0

bunduki

KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na sialaha wameteka eneo la mpaka wa Tanzania na Rwanda katika Kijiji cha Benako wilayani Ngara mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo na kujeruhi mtu mmoja aliyekuwa dukani huku wakipora fedha kwenye maduka na taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa chanzo cha taarifa hiyo, inasemekana baada ya watu hao waliokuwa na silaha (bunduki) kufika katika kijiji hicho walikiteka kwa muda wa saa tatu huku wakifyatua risasi ili kuwatia woga wakazi wa eneo hilo, ndipo wakatekeleza adhma yao ya kuingia kwenye maduka ya wafanyabiashara na taasisi mbalimbali kisha kupora kiasi cha fedha ambacho hakijajulikana.

Katika tukio hilo hakuna mtu aliyeripotiwa kuuawa.

Baada ya kutekeleza tukio hilo majambazi hao walitokomea kusiko julikana na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linafanya kila jitihada ili kuwatia nguvuni watu hao.

Leave A Reply