The House of Favourite Newspapers

Majeneza Yenye Miili ya Watu Yaelea Mitaani

0

KATIKA hali ya kushangaza, majeneza yenye mabaki ya miili ya watu yameonekana yakielea na kuzagaa mitaani katika Jimbo la Louisiana nchini Marekani kufuatia makaburi kufukuliwa na maji ya mafuriko.

 

Tukio hili limejiri ikiwa ni wiki chache tangu majeneza hayo yaliposombwa na maji kutoka kwenye makaburi kufuatia mafuriko yaliyoambatana na Kimbunga Ida.

 

Inakadiriwa kuwa majeneza 30 hadi 40 yameonekana yakiwa yamezagaa huku makaburi yakiwa tupu, baadhi ya watu wanaendelea kutafuta majeneza ya ndugu zao ili wazike tena.

Watu wanne wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 7,000 kunusurika vifo huku wakiokolewa kutokana na mvua hiyo kubwa.

Leave A Reply