The House of Favourite Newspapers

Majirani Wafunguka: Hamza Alikuwa Mtu wa Kawaida – Video

0

KUFUATIA tukio la jana Agosti 25, 2021 la kijana mmoja anayetajwa kwa jina la Hamza mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam kuvamia maaskari akiwa na silaha kisha kua askari polisi wawili na mlinzi mmoja wa Kampuni ya SGA huku akijeruhi watu sita kabla ya yeye kuuawa, Global TV Online imefika nyumbani kwao na kijana huyo kujua undani zaidi.

 

Majirani wa familia hiyo wamefunguka mengi namna walivyomfahamu Hamza huku wakisema hawakudhania kama angefanya tukio hilo kwani wamekuwa wakimuona kama mtu wa kawaida tu na hakuwa na dalili za tabia za kihalifu.

 

“Hamza hakuwa mzungumzaji kwa sana, hana matatizo na mtu yoyote nimeshangaa sana kwa lile tukio, ukikaa naye ni mtu wa kawaida sema hana mazungumzo mengi.

 

“Namfahamu sana tangu makuzi yake ya udogoni ila kuna muda aliondoka na juzi juzi alirudi akawa anapita na pikipiki yake hapa ila tukio hili limenishtua sana.” amesema Omary, Jirani yake Hamza, aliyezua taharuki jana.

 

“Mara ya mwisho kuja hapa kununua chips ilikuwa Jumatatu na alikuja hapa akaagiza chakula akala tukawa tunapiga nae story za kawaida tu hapa.” amesema Issa muuza chips Upanga, mahali ambapo Hamza alikuwa anaenda kuchukua chips.

TAZAMA HAPA FULL VIDEO

Leave A Reply