The House of Favourite Newspapers
gunners X

Majirani Wasikitikia Mjengo Wa Mama Lulu

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Huyu binti yake Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa gerezani Segerea jijini Dar akitumikia kifungo cha miaka miwili kufuatia kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia mwigizaji Steven Kanumba, mama mzazi wa mrembo huyo, Lucresia Karugila anadaiwa kuususia mjengo wa bintiye huyo hivyo kusababisha majirani kuusikitikia.

Mjengo wa kifahari  wa Lulu uliopo maeneo ya Kimara-Temboni, Kata ya Saranga jijini Dar.


Mjengo huo wa kifahari upo maeneo ya Kimara-Temboni, Kata ya Saranga jijini Dar. Kwa mujibu wa majirani hao wanaokaa karibu na mjengo huo walioomba hifadhi ya majina, tangu mwanaye atupwe jela, mama Lulu hajawahi kwenda kwenye mjengo huo na sasa umegeuka kuwa makazi ya ndege, jambo ambalo linawasikitisha.

 

Ijumaa lilifika kwenye mjengo huo na kukuta ukiwa umetelekezwa na kuzungumza na majirani hao ambao walieleza kuwa, kipindi cha nyuma wakati Lulu akiwa uraiani, alikuwa anakwenda kwenye mjengo huo, lakini baadaye naye alikata mguu.

 

“Yupo kijana mmoja hapa huwa anakuja mara chache kwa ajili ya kupalilia majani, lakini kwa sasa ana muda mrefu hajaonekana kiasi kwamba majani yameota kila kona.

Muonekano wa nyumba hiyo.

“Kwa mfano, kwa upande wangu mimi huwa ninawasiliana na mama Lulu umeme ukikatika ili kumpa taarifa na lolote lile linalotokea hapa huwa ninamjulisha,” alisema mmoja wa majirani hao.

Jirani huyo alieleza kuwa, tangu mjengo utangazwe kupangishwa miezi kadhaa iliyopita hajawahi kutokea mpangaji na kuna aliwahi kusikia unataka kuuzwa.

 

Baada ya Ijumaa kujionea mazingira yenyewe na kuzungumza na majirani wawili-watatu, lilimtafuta mama Lulu ili kuzungumzia hali ya mjengo huo.

Alipotafutwa kwa njia ya simu, mama Lulu ambaye alizawadiwa mjengo huo na bintiye huyo katika siku yake ya kuzaliwa ya mwaka 2015 alifunguka:

Nyumba ikiwa imezungukwa na majani.

“Sijautelekeza mjengo wangu, pale kuna mwanangu anaishi. Siupangishi na wala sihitaji komenti yoyote kutoka kwa mtu yeyote kwa sababu nyumba ni yangu.”

 

Mama Lulu alipoelezwa na gazeti hili kwamba lilifika eneo la tukio na kubaini kwamba hakuna mtu anayeishi kutokana na hali halisi, mama huyo alibonyeza kitufe chekundu cha simu na kuingia mitini.

Alipopigiwa simu kwa mara nyingine, wala mama Lulu hakujisumbua kupokea.

Boniphace Ngumije na Ally Katalambula

Comments are closed.