The House of Favourite Newspapers

Kumbe Mabeki Walimzingua Pluijm Singida United

KOCHA wa Singida United, Hans van Der Pluijm raia wa Uholanzi, amesema anaamini kipigo cha mabao 4-0 kutoka Simba kwa kiasi fulani kimechangiwa na safu yake ya ulinzi.

Singida United ambao walikuwa wageni wa Simba, juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam walifungwa idadi hiyo ya mabao katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Pluijm alisema safu ya ulinzi na ile ya kiungo zilifanya makosa kadhaa jambo ambalo lilichangia wao kupokea kipigo hicho kizito.

“Tulifanya makosa kadhaa hasa katika safu ya ulinzi na ile ya kiungo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kwetu kupoteza.

 

“Lakini tunachukua makosa hayo na kwenda kuyafanyia kazi katika michezo yetu mingine, hii haikuwa siku yetu hata kidogo kwani kama unavyoona tumepoteza tena kwa kipigo kikubwa,” alisema Pluijm ambaye aliwahi kuinoa Yanga.

 

Wakati huohuo, beki wa Singida, Maliki Antri raia wa Ghana, amesema hawapaswi kutupiana lawama juu ya kipigo hicho bali wanajipanga kwa michezo ijayo. Keshokutwa Jumatatu, Singida United itacheza na Majimaji ugenini mjini Songea.

Said Ally, Dar es Salaam

Comments are closed.