The House of Favourite Newspapers

Majuto Adaiwa Kumtokea Mkewe

DAR ES SALAAM: Baada ya maneno mengi huku ndugu wa aliyekuwa mumewe, Amri Athuman ‘King Majuto’ wakidaiwa kumnyima huduma muhimu kama chakula, mjane wa mzee huyo aliyekuwa kinara wa vichekesho Bongo, Aisha Yusuf anadaiwa kutokewa na mzee huyo kwani hafurahishwi na vitendo vinavyoendelea.

 

Kufuatia madai hayo huku mama huyo akiwa ameondoka Tanga na kurejea kwa wazazi wake jijini Dar, gazeti hili lilimtafuta Aisha ambaye katika mahojiano maalum alielezea hali hiyo;

Risasi Jumamosi: Habari mama, unaendeleaje?

Aisha: Sijambo, naendeelea vizuri.

Risasi Jumamosi: Kuna tofauti gani ya kimaisha tangu Mzee Majuto aondoke?

Aisha: Lazima kuwe na utofauti ingawa ninamshukuru Mungu mimi sijambo.

Risasi Jumamosi: Kuna madai kuwa Mzee Majuto amekutokea hivi karibuni baada ya matatizo yako, je, unalizungumziaje hilo?

Aisha: Hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwa sababu mimi nilikuwa karibu naye. Kwa yeyote anayefiwa, atakutana na hali hii ingawa ni mapema mno kuliongelea.

 

Risasi Jumamosi: Kwa nini unasema ni mapema mno? Je, hakuna chochote amekuambia katika kukutokea huko?

Aisha: Sina la kusema zaidi ya hapo kwani hata watoto bado yupo machoni mwao wanamuona, mara nyingi hata kiimani, kinachoondoka ni kiwiliwili tu, lakini roho bado inakuwepo, kwa hiyo kusema Majuto hajanitokea siwezi kwani namuona wakati wote.

MADAI! FAMILIA YAMSUSA MKE WA MAJUTO & WATOTO WAIKE, ASIMULIA – VIDEO

Kingine nisema tu Majuto sidhani kama anaweza kuniambia kitu kipya kwani wakati kabla ya kukata roho alishanipa maelekezo ya kutosha tu ambayo kama mama nimeyaelewa.

Risasi Jumamosi: Ni maneno gani hayo aliyokuambia ambayo unaamini yanatosha kuelewa?

Aisha: Aliniambia niwachukue watoto wake wadogo niwarudishe nyumbani kwa wazazi wangu, walelewe hapo hadi wakue na hapo watakuwa na amani sana kuliko kwa ndugu zake. Naamini maneno hayo hata ukiambiwa wewe utaelewa.

 

Risasi Jumamosi: Kwa hiyo anapokutokea kwa sasa anakuambia nini?

Aisha: Hanitokei kwa maneno yoyote bali namuona kwa sababu ya ukaribu tuliokuwa nao mimi na yeye kama mkewe, kitendo ambacho ni kawaida kutokea kwa yeyote.

Risasi Jumamosi: Pole na kwaheri

STORI:Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi.

BABA MKWE WA MAJUTO: WALIDAI URITHI HOSPITAL KABLA HAJAFA – VIDEO

Comments are closed.