The House of Favourite Newspapers

Makaburi Ya Halaiki Kujengwa Gaza

0

Wapalestina wanaoishi katika Ukanda wa Gaza, wameanza kuchimba makaburi ya halaiki kuwazika ndugu zao, kutokana na ongezeko kubwa la watu wanaopoteza maisha kila siku kutokana na mapigano kati ya Israel na Hamas.

Kutokana na ardhi kubwa ya Palestina kuwa mchanga, mmoja kati ya wachimba makaburi katika Makaburi ya Deir el Balah, Sadi Barka ameliambia Shirika la Utangazaji la VOA kwamba wanalazimika kupanga matofali ili kuzuia mchanga usipoteze mwonekano wa makaburi hayo.

Ameongeza kwamba kutokana na idadi kubwa ya watu waliopoteza maisha, wanalazimika kuchimba makaburi ya pamoja kwani ni vigumu kuchimba kaburi mojamoja.

Leave A Reply