The House of Favourite Newspapers

Makambo Awataja Fei Toto, Tshishimbi Siri ya Mabao Yake Yanga

MSHAMBULIAJI mpya hatari hivi sasa wa Yanga, Mkongoman, Heritier Makambo, ametoa pongezi kwa viungo wa timu hiyo, Feisal Salim ‘Fei Toto’ na Papy Tshishimbi ambao ndiyo wana siri ya mabao yake anayofunga.

Kauli hiyo, aliitoa ikiwa ni saa chache baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 juzi Al­hamisi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Mkongoman huyo hivi sasa amepata umaarufu mkubwa katika msimu huu kutokana na kasi yake aliyoanza nayo ya kufunga mabao, pia uwezo wake wa kupambana na mabeki wa timu pinzani ambapo tayari amefunga mabao sita.

Akizungumza na Championi Ju­matatu, Makambo alisema pongezi nyingi ziende kwa viungo wake hao am­bao wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kumtengenezea mabao.

 

Makambo alisema, kama viungo hao wakiendelea kucheza pamoja kwa muda na kuzoeana, basi ana matarajio makubwa ya kufun­ga mabao mengi kutokana na aina ya pasi wanazompatia.

“Pongezi nyingi ziende kwa viungo wangu wachezeshaji Fei Toto, Tshishimbi, Rap­hael (Daudi) na wengine ambao wamekuwa wak­itimiza majukumu yao ya kunichezesha, kwa maana ya kunipigia pasi na krosi nzuri za kufunga mabao.

 

“Ukiangalia mechi (dhidi ya Mtibwa), utaona kazi kubwa iliyofanywa ya viungo wakabaji na wachezeshaji ambao wali­tutengenezea nafasi nzuri za kufunga mabao, pia kupunguza mashambulizi kwa maana ya kukaa na mipira kwa lengo la kutoipoteza.

“Ni matarajio yangu kuona viungo hao wakiendelea ku­timiza majukumu yao kwa faida ya timu katika kuwapa furaha mashabiki wetu wa Yanga kwa kupata matokeo mazuri,” alisen­ma Makambo.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.