The House of Favourite Newspapers

MAKAMU WA RAIS WA TANZANIA, SAMIA SULUHU AWASILI, ZANZIBAR LEO

0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Alipowasili Katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar

Makamu wa rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewasili leo jioni katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwa ajili ya kuhudhuria  hafla mbili za kitaifa, kuhitimisha kilele cha Mwenge na kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha baba wa Taifa, Mwl Julius Nyerere, zikazofanyika kesho katika uwanja wa Aman uliopo katika mkoa wa Mjini Magharibi.

RC wa DSM, Paul Makonda Akisalimiana na RC wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahmoud

Mama Samia na RC Makonda wamepokelewa na mwenyeji wao, mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ambaye aliwashukuru kwa kuwasili kwao Zanzibar na kuahidi kushirikiana nao kikamilifu katika shughuli ya kesho.

Uwanja wa Taifa wa Zanzibar, Aman

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply