The House of Favourite Newspapers

WAFADHILI WAKABIDHI MSAAADA WA VYOO KIGAMBONI

0

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) pamoja na Shirika la Sanitation and Water Action (SAWA), kwa pamoja yamekabidhi  matatu ya vyoo 20  yaliyokarabatiwa kwa Shule ya Msingi Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Vijibweni katika maadhimisho ya Siku ya Kunawa Mikono Duniani yaliyoenda sambamba na makabidhiano ya vyumba hivyo, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameyashukuru mashirika hayo kwa msaada huo mkubwa walioutoa.

 

Mwita ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vijibweni, amesema pamoja na msaada huo waliopewa, bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili wananchi wa Vijibweni na Jiji la Dar es Salaam kwa jumla, ikiwemo uhaba wa vyoo, vyumba vya madarasa, ofisi za walimu na miundombinu mingine, na kuwaomba wafadhili hao, waendelee kutoa misaada.

 

“Nawashukuru sana, mmefanya kazi kubwa lakini msiishie hapo, leo hii mpo kwenye Kata ya Vijibweni lakini zipo shule nyingi ambazo zina uhaba wa vyoo, nitumie nafasi hii kuwaomba tena pamoja na wadau wengine ambao wanaweza kutusaidia katika hili,” alisema Mwita.

 

Aidha katika hatua nyingine, Meya Mwita amewahakikisha walimu wa Shule ya Msingi Vijibweni kuwa kutokana na changamoto za ofisi za walimu katika shule hiyo, hadi ifikapo Agosti, 2018 atakabidhi ofisi mpya shuleni hapo.

 

“Kwenye mambo ya maendeleo, serikali inaendelea kufanya kwa nafasi yake, lakini pia wazazi tusaidiane katika ujenzi wa shule, tumeshapata ekari saba kwa jitihada zangu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ambapo kuanzia mwakani (2018), tutaanza kujenga shule,” alisema Mwita.

 

Kwa upande wake, Mtaalam wa Huduma za Maji, Afya na Usafi wa Mazingira wa Unicef, John Mfungo amempongeza Meya Mwita kwa ushirikiano wake tangu kuanza kwa mradi huo na kusema kuwa alikuwa akitumia muda mwingi na mwananchi wake kuonesha ushiriki na hivyo kufanikisha kukamilika kwa ujenzi huo.

 

Leave A Reply