The House of Favourite Newspapers

Makocha Wanne Kumrithi Solskjaer Man U

0

KLABU ya Manchester United imewaweka makocha wanne kwenye uangalizi ili waweze kuchukua nafasi ya kocha wao wa sasa Ole Gunnar Solskjaer.

 

United wanaweza kumtimua kocha wao huyo muda wowote kuanzia sasa na nafasi yake inatajwa kuwa itachukuliwa na mmoja kati ya makocha hao.

 

Man wameshindwa kufanya vizuri kwenye michezo ya Ligi Kuu England iliyopita ambapo hivi karibuni walijikuta wakilala kwa mabao 5-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Dimba la Old Trafford.


Mbali na Antonio Conte
ambaye anatajwa sana kuchukua nafasi ya Ole timu hiyo inawawinda pia Brendan
Rodgers wa Leicester
City, Erik ten Hag wa Ajax pamoja na Zinedine Zidane ambaye ni kocha wa zamani wa
Real Madrid.


Hata hivyo,
wachambuzi wa masuala ya soka la England wanasema kuwa Conte ndiye anayepewa nafasi kubwa
zaidi ya kuichukua timu
hiyo kama itapoteza mchezo ujao wa ligi England.


Endapo timu hiyo
itamkosa Conte basi kuna uwezekano mkubwa ikabadilishia gia kwa Zidane na ikishindikana ndiyo itawafuata hao wengine.

Leave A Reply