The House of Favourite Newspapers

Makonda Achafua Hali Ya Hewa Mbele Ya Rais Samia-Atishia Kuwataja Vigogo Wanaomtukana Rais Mtandaoni – Video

0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema anawafahamu wanaolipa watu ili kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kumkatisha tamaa na kuwataka kuacha mara moja.

“Nafahamu wenye maneno na hawaishi kusema maneno, lengo lao ni kukatisha tamaa (Rais Samia).

Tena wengine umetupa nafasi humu ndani ya uongozi wako na nitumie fursa hii kuwaambia hasa kaka zangu mnaotuma watu na kuwalipa kumchokoza mama yangu (Rais Samia).

Ninawajua na ninyi mnanijua. Narudia tena, hasa kaka zangu mnaotuma na kulipa watu kumchokoza Mama yangu Samia nawajua na ninyi mnanijua.

Rais (hawa watu) kwa majina yao nawajua na leo tarehe 12 (Aprili, 2024) nataka iwe mwisho kuwatuma watu hao wanaokutukana kwenye mitandao ya kijamii. Jumatatu ikiendelea nakutajia majina. Wengine ni mawaziri na wengine wanapewa nguvu na watu tunaowaheshimu. Naomba iwe mwisho. Tumwache Dkt. Samia afanye kazi aliyopewa na Mungu,” amesema Makonda

Makonda amesema hayo wakati akishiriki kumbukizi ya miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine, Monduli mkoani Arusha.

Leave A Reply