The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AKAGUA MIRADI YA BARABARA KIGAMBONI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa kwanza kulia) akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Wilaya ya Kigamboni. Wa tatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri.
Makonda akiwasikiliza wananchi wa maeneo ya Kigamboni.
...Akiangalia baadhi ya miundombinu ya barabara ambayo tayari imekwishajengwa eneo la Kigamboni kutokea daraja la Mwalimu Nyerere.
Miundombinu ya barabara ikijengwa.
Baadhi ya barabara zikiwa tayari ujenzi wake.
Makonda akiendelea kuangalia barabara zinazojengwa.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya Barabara na Madaraja inayotekelezwa na Serikali kwenye Wilaya ya Kigamboni ambapo kukamilika kwake kutafanya mji wa kigamboni kuwa wa kisasa zaidi.

 

 

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na Makonda ni ujenzi wa Barabara ya njia sita za magari kuelekea Daraja la Mwalimu Nyerere yenye urefu wa Km 2 pamoja mzunguko wa magari (Round about) yenye ukubwa wa meter 250 kuelekea Feri Meter 250 kuelekea Kibada ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Oktoba 31 mwaka huu.

 

 

Aidha Makonda ametembelea ujenzi wa Barabara ya KKKT na mitaro ya maji yenye urefu wa Mita 275, Barabara ya Hospital ya Vijibweni Mita 800 kutoka Kibada, Barabara ya Kijaka-Mwasonga Km 8, Mwasonga-Kibada Km 16 Kimbiji-Pembamnazi, Daraja la Puna eneo la Buyuni na Daraja la Kibugumo pia katika  Kata ya Gezaulole ambapo miradi hiyo ipo hatua za mwisho kukamilika.

 

 

Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo na kuwahimiza TANROAD na TARURA kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati ili wananchi waendelee kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano.

 

 

Pamoja na hayo Makonda amesema wamejidhatiti kuhakikisha Kigamboni inakuwa na Barabara za Lami, maji ya kutosha na umeme kwaajili ya viwanda, makazi na showroom kubwa Afrika Mashariki na kati.

 

Comments are closed.