The House of Favourite Newspapers

NHC KUJENGA OFISI ZA EWURA DODOMA

Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Injinia Nyirabu Musira akimkabidhi  Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio mchoro wa jinsi jengo la Makao Makuu ya Ewura Dodoma litakavyokuwa.

Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio na wafanyakazi wengine wa Shirika la Nyumba la Taifa wakiwa ndani ya ofisi za NHC Dodoma.
Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio na Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Nyirabu Musira wakielekea kwenye eneo la tukio.
Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wale wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dodoma wakikagua eneo la mradi. 
Watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa na Wale wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Dodoma wakikagua eneo la mradi. 
Mchoro wa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

 

Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Injinia Nyirabu Musira leo  amemkimkabidhi  Mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Haikamen Mlekio mchoro wa jinsi jengo la Makao Makuu ya Ewura Dodoma litakavyokuwa.

 

 

Makabidhiano  hayo ya  Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Mamlaka hiyo yamefanyika jijini Dodoma.

 

Shirika la Nyumba limepewa kandarasi ya kujenga jengo hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 ambalo litakuwa makao makuu ya Mamlaka hiyo nchini. NHC imepewa dhamana ya kuusanifu, kujenga na kuusimamia mradi huo.

Comments are closed.