MAKONDA ALIVYOMMALIZA MOBETO KWA WEMA

AMEMMALIZA Mobeto (Hamisa)! Ndivyo walivyosikika wapenda ubuyu wa mjini waliohudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mwigizaji Wema Isaac Sepetu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaja mrembo huyo kuwa ndiye mrembo wa taifa anayependwa zaidi (Tanzania Sweetheart).

 

KWA NINI AMEMMALIZA?

Mashabiki hao wa burudani waliibua kelele hizo kufuatia ule ubishi uliotikisa mitandaoni ukidai Wema hastahili kuitwa Tanzania Sweetheart tena na badala yake cheo hicho kwa sasa ‘kinamfiti’, mwanamitindo Mobeto.

 

“Yaani kwa kweli amemmaliza Mobeto, hivi wewe unafikiri kwa kauli hii, wale mashabiki wa Mobeto wanapata wapi ujasiri tena wa kumuita Tanzania Sweetheart kama mwenye mkoa wake ameshasema anamtambua Wema tu ndiye Tanzania Sweetheart kuna nini tena,” alisikika mpenda ubuyu aliyejitambulisha kwa jina la Jesca Kibajaj na mwenzake aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce akadaikia:

 

“Ndiyoo, baba Makonda ameshamaliza ubishi, haijalishi kasema kama maoni yake binafsi au vipi, lakini kwa vile ni kiongozi, kauli yake ina uzito tosha wa kumzima Mobeto.”

 

MAKONDA ALILIAMSHAJE?

Makonda baada ya kuhudhuria bethidei ya Wema katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita, wakati anatoka ndipo mapaparazi walimpovaa kwa maswali.

Awali, mapaparazi walimtaka Makonda atoe mtazamo wake kuhusiana na filamu ya D.A.D ambayo Wema aliizindua siku hiyo ndipo Makonda alipoanza kumsifia mrembo huyo kuwa amefanya kazi hiyo nzuri aliyoshirikiana na msanii wa Ghana, Van Vicker.

“Hii ni kazi nzuri sana ambayo Wema amefanya na Van Vicker na labda niseme tu, ninampongeza sana Wema kwa kazi hii na ameonesha uwezo wa hali ya juu,” alisema Makonda.

HAPA NDIPO ALIPOMMALIZA MOBETO

Alipoulizwa kuhusu ishu ya umalikia wa Tanzania Sweetheart kwamba nani anastahili kubeba ‘taito’ hiyo, bila kupepesa macho, Makonda alimtaja Wema.

“Wema ndiye Tanzania Sweetheart wa ukweli na hilo jina hakujipa mwenyewe, amepewa na mashabiki siyo hao wengine ambao nao eti wanajiita masweet heart, mimi ninachojua Wema ndiye Tanzania Sweetheart siyo hao wanaoiga,” alisema Makonda bila kumtaja moja kwa moja Mobeto.

 

Lakini hata hivyo, wambeya waliokuwepo eneo hilo, walijiongeza kwa kusema maneno hayo ya Makonda yalikuwa yanamlenga Mobeto moja kwa moja kwani ndiye ambaye hivi karibuni aliibua mjadala mitandaoni kwa mashabiki wake kumpigia debe awe Tanzania Sweetheart.

 

ANAMZUNGUMZIAJE MOBETO?

Alipobanwa ili angalau amzungumzie mwanamitindo Mobeto kwa namna yoyote ile, Makonda alisema hakuna anachoweza kumzungumzia na kukatisha mahojiano kisha kuingia kwenye gari lake na kuondoka.

 

AIBUA YALIYOLALA

Kauli hiyo ya Makonda kuonesha ‘mahaba’ yake ya wazi kwa Wema na kutomzungumzia Mobeto iliibua upya mjadala mitandaoni kwa watu kuanza tena kuzungumzia ishu hiyo ambayo ilishaanza kupoa.

Mashabiki wa Wema ambao kipindi cha nyuma walionekana kuzidiwa nguvu na wale wa Mobeto, walianza kupata nguvu upya na kupeleka mashambulizi kwa Mobeto.

“Ana lipi yule (Mobeto) hadi awe Tanzania Sweetheart?” alichangia mmoja wa mashabiki wa Wema katika mtandao wa Instagram.

Hata hivyo, mashabiki wa Mobeto nao waliibuka kujibu mashambulizi hayo licha ya kuonekana wamenyong’onyezwa na kauli ya Makonda.

MATUKIO KAMA YOTE!

Kwenye bethidei ya Wema, matukio mbalimbali yalijitokeza ambayo yalizua gumzo.

HARMORAPA VS MADAM

Minongoni mwa matukio hayo ni pamoja na lile la msanii wa Bongo Fleva, Hamorapa kutinga na ua kisha kumkabidhi Wema akidai anampenda.

WOLPER, UWOYA NA MABODIGADI

Tukio la warembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya na Jacqueline Wolper kuingia ukumbini wakiwa na mabodigadi wao nalo lilibua gumzo kwa mashabiki ambao hawajawazoea kuwaona wakiwa na walinzi hao.

“Mh! Hii kiboko Bongo Movies nao wameona wasipitwe na mambo haya, hataree,” alisikika shabiki mmoja aliyehudhuria hafla hiyo ambaye hakutaka kujitambulisha.

Uwoya alitisha zaidi baada ya kuonekana na Mwarabu Fighter, baunsa ambaye aliwahi kuwa wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kisha wakazinguana huku ikidaiwa kwa vyovyote kuna kitu nyuma ya pazia.

MAMA WEMA, MAMA DIAMOND NDANI

Mama Wema, Miriam Sepetu naye alikuwa ni miongoni mwa mamia ya watu waliofika kumpa kampani Wema katika tukio hilo muhimu la bintiye bila kumsahau, ‘mama mkwe’ wa zamani wa Wema, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’.

Bi Sandra alisema katika hafla hiyo hajamuwakilisha mwanaye Diamond bali alifika kuonesha mapenzi yake kwa Wema.

WAZIRI SHONZA ATOKELEZEA

Kuonesha kwamba usiku huo ulitambulika pia kiserikali, mbali na uwepo wa mkuu wa mkoa wa Dar, alikuwepo pia Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza.

Toa comment