Makonda Apokea Misaada ya Waathirika wa Mafuriko Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo Aprili 26, 2018, amepokea msaada wa magodoro, neti na vyakula kutoka kwa taasisi mbili tofauti zilizotokea Zanzibar; moja ni Abdullah Aid Emergency Appeal na Darul Irshad Islamic Centre kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko waliopoteza mali zao hivi karibuni kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo kwa zaidi ya siku tatu.
Baada ya kupokea msaada huo, Makonda amezishukuru taasisi hizo na kuweka wazi kuwa misaada hiyo itakwenda kwa waathirika wa mafuriko ambao nyumba zao hazipo mabondeni, kwani wale ambao wanaishi mabondeni wamekiuka agizo la serikali la kuwataka wahame kabla ya mafuriko kuwakuta.
Comments are closed.