The House of Favourite Newspapers

Makonda Atoa Maagizo: Viongozi wa Mwendokasi Niwakute Kimara Stand

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hafurahishwi na namna mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini humo unavyoendeshwa na kugeuka kuwa kero kwa wananchi badala ya kuwa msaaba kama yalivyokuwa matarajio ya Serikali na wananchi wake.

 

Makonda amesema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwataka viongozi wanaosimamia mradi huo akutane nao kesho asubuhi katika stendi ya mabasi ya Mwendokasi eneo la Kimara.

 

“Sifurahishwi na namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh. Rais Magufuli ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu.

 

“Kwa sababu hizo nimeagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi niwakute Kimara Stand ya mwendokasi kesho saa 12:30 asubuhi wanieleze kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi.

 

“Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi kwa kero hii na niwaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukutane mapema asubuhi mwendokasi kimara.” ameandika Makonda.

 

Mapema leo Oktoba 10 katikarkituo cha mabasi hayo Kimara kimeonekana kuwa mlundikanao wa abiria wengi hadi kusababisha baadhi ya0 kuzirai kwa kukosa hewa ya kutosha huku wengine wakigombania kwa kupita dirishani mara yanapotokea.

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.