The House of Favourite Newspapers

MALAIKA AELEZA KUPOTEA KIMUZIKI, KUMWANIKA MPENZI WAKE

Image result for Diana Exavery ‘Malaika’.
Diana Exavery ‘Malaika’.

KAMA wewe ni mdau wa Muziki wa Bongo Fleva na hakuna ‘hits song’ ambayo imekupita, bila shaka masikio yako yatakuwa yalishawahi kusikia Ngoma ya Sare Sare au Rarua Rarua kutoka kwa msanii Diana Exavery ‘Malaika’.

Malaika ambaye alichipukia kwenye kolabo ya Uswazi Take Away akiwa na Chegge, kwa muda sasa amepotea kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva akiwa bado yupo ‘hot’.

Showbiz Xtra kama kawaida limeingia chimbo na kumuibua ambapo ametaja sababu zilizomfanya kuwa kimya kwenye mambo ya muziki japokuwa anaamini kuwa mashabiki wake wataendelea kuwepo walewale kwa kuwa yeye ni yeye na ataendelea kuwa yeye. Huyu hapa;

SHOWBIZ EXTRA: Mashabiki wangependa kujua umepotelea wapi maana umekuwa kimya kidogo?

Malaika: Nipo na unajua nje ya muziki kila mtu ana majukumu yake mengine lakini nipo.

SHOWBIZ EXTRA: Sasa ukipumzika kidogo kama hivyo mashabiki si unawapoteza?

Malaika: Unajua kila mwanamuziki anakuwa na ladha yake tofauti na mimi siwezi kuwa yule na yule hawezi kuwa mimi hata siku moja.

SHOWBIZ EXTRA: Sasa hivi unaonekana zaidi kwenye kampeni za Sickle Cell, kwa nini umeamua kujiingiza huko?

MALAIKA: Nimeamua kwa sababu ni vyema pia kujiingiza kwenye kazi za kijamii na ndivyo ninavyofanya sasa.

SHOWBIZ EXTRA: Uliamua mwenyewe au walikufuata uweze kuungana nao kwenye kampeni hiyo?

Malaika: Walinifuata wenyewe na kuwakubalia kwa moyo mmoja kwa sababu hata huko napotoka kwenye familia yangu magonjwa hayo yapo.

SHOWBIZ EXTRA: Kuna kipindi mashabiki walijua umeamua kuhamishia muziki wako nje ya nchi, kwa sababu kila mara ulikuwa ukipiga shoo huko kwa nini ilikuwa hivyo?

MALAIKA: Unajua kila mwanamuziki anapenda kujipanua kupitia anachokiimba hivyo hiyo ilikuwa moja ya njia nyimbo zangu zisikike popote na ndio maana ilikuwa hivyo.Image result for Diana Exavery ‘Malaika’.

SHOWBIZ EXTRA: Kutokana na kufanya hivyo, ulifanikiwa ulichokuwa ukitaka?

MALAIKA: Ndio na mpaka sasa mashabiki bado wananialika kufanya shoo huko.

SHOWBIZ EXTRA: Lakini kuna baadhi mashabiki wanaamini mpenzi wako amekukataza kuimba.

MALAIKA: Hakuna wa kunikataza kuimba maana hata familia yangu haiwezi kufanya hivyo.

SHOWBIZ EXTRA: Baadhi ya mastaa wamekuwa wakiweka uhusiano wao wazi lakini wewe hakuna ambaye anajua mpenzi wako ni kwa nini?

Malaika: Sidhani kama ni sawa kuweka kila kitu chako binafsi nje, maana wanachotaka mashabiki ni kazi yako na sio uhusiano wako.

SHOWBIZ EXTRA: Huoni kama kutomuweka wazi mpenzi wako kunakufanya kupata usumbufu mkubwa.

Malaika: Usumbufu upo mkubwa na ukizingatia ni msichana mzuri lakini hiyo haifanyi nimuweke wazi mpenzi wangu.

SHOWBIZ EXTRA: Asante sana

Malaika: Asante sana.

Comments are closed.