Kartra

Malkia Aitakia Heri England

KIKOSI cha Kocha Gareth Southgate cha England kimepokea ujumbe kutoka kwa Malkia Elizabeth II kabla ya Fainali ya Euro 2020 dhidi ya Italia leo, saa 4:00 usiku.

 

England wamefika Fainali ya Euro kwa mara ya kwanza, wakati miaka 55 imepita tangu kuingia katika fainali ya mashindano makubwa baada ya kufanya hivyo walivyotwaa Kombe la Dunia mwaka 1966 .

 

Malkia Elizabeth II alihudhuria siku hiyo, wakati England ikiifunga Ujerumani Magharibi mabao 4-2 kwenye Fainali ya Kombe la Dunia ya 1966.

 

Katika mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi, Southgate amesema; “Tumepokea barua ya kututakia kila la heri kutoka kwa Malkia na Waziri Mkuu kwenda kwa timu nzima na kutambuliwa kwa wachezaji na wafanyakazi wote.

 

“Tulikuwa na mapokezi mazuri tukiondoka uwanja wa mazoezi wa St George na vijiji vyote vilijipanga njiani. Unapata hisia zaidi ya kile kinachoendelea nje ya kambi yetu.

 

“Tumefika fainali na tuko hapa kushinda. Ni muhimu jinsi tunavyowakilisha watu na urithi huo upo, lakini tunataka kuleta kombe nyumbani kwa kila mtu.”

 


Toa comment