The House of Favourite Newspapers

Malumbano ya Flash Yaibuka Mahakamani

0

MALUMBANO ya kisheria leo yameendelea katika Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita, ambapo mawakili wake wamepinga kupokewa kwa flash kama kielelezo katika kesi hiyo.

 

Malumbano hayo yalimfanya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo jana Oktoba 28, 2021 kuiahirisha hadi jumatatu atakapotoa uamuzi mdogo wa kupokewa au kutopokewa kwa flash hiyo.

 

Awali mawakili upande wa utetezi walipinga kupokewa kwa kielelezo hicho kilichotolewa na shahidi wa nane, Johnson Kisaka ambaye ni Ofisa Uchunguzi kutoka katika maabara ya uchunguzi wa kielekroniki ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

 

Wakili wa Utetezi, Moses Mahuna amedai sheria inataka upande wa Jamhuri wanapotaka kutoa kielelezo ni lazima upande wa pili wakipate ili wapate muda wa kupitia na kuona kama wanatoa pingamizi au la.

Leave A Reply