The House of Favourite Newspapers

MAMA AFUNGUKA UKARIBU WA WEMA , DIAMOND !

DAR ES SALAAM: Mama wa msanii wa Bongo Movies, Wema Sepetu, Miriam, amefungukia ukaribu walionao bintiye na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa sasa kuwa ni wa kirafiki tu na kamwe hawawezi kurudiana tena.  

Akichezesha taya na Amani baada ya mwanahabari wetu kumuuliza kama atakuwa tayari kupokea posa ya Diamond kama atajirudi na kuomba nafasi nyingine kwa bintiye, alisema wawili hao imebaki stori.

 

“Wewee, sikiliza nikwambie bwana, Wema na Diamond kwa sasa wamebaki kuwa marafiki tu. Haiwezi kutokea tena wakarudiana. Mimi ndiyo namjua Wema vizuri, ana moyo wa aina yake ndiyo maana unaona pamoja na kuwa wameshaachana lakini bado wanakuwa karibu, wanashirikishana mambo yao kiroho safi,” alisema mama Wema.

 

Aliongeza kuwa, hivi karibuni watu wamekuwa wakizusha kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna uwezekano Wema akarudiana na Diamond lakini hilo kamwe haliwezi kutokea.
“Wema ana maisha yake sasa hivi, Diamond ana yake, kamwe hawawezi tena kurudiana,” alisisitiza mama Wema.Image result for navy kenzo na sallam sk

Wema na Diamond waliwahi kuwa wapenzi kwa miaka kadhaa kisha wakamwagana na kurudiana kabla Diamond hajachomoka na kwenda kukita nanga kwa mrembo wa Kiganda, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aliyebahatika kuzaa naye watoto wawili kisha kumwagana naye, mapema mwaka huu.

Comments are closed.