The House of Favourite Newspapers

Mama Afungwa Jela kwa Kuruhusu Wanaume Kumbaka Mwanaye

MWANAMKE Azzie Watson (25) wa Independence, Kansas City, Marekani, ameshitakiwa kwa kuuruhusu wanaume kumbaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka miwili.

Mahakama iliambiwa kwamba mtuhumiwa huyo alikuwa kila mara anasema alimpeleka mtoto wake huyo kwenye nyumba fulani ambako alibakwa mara tano.  Maneno hayo yanadaiwa yalinaswa na rafiki yake wa kiume kwenye kinasa sauti.

Watson alikana madai hayo, lakini pia akasema hajui ni kwa nini mtoto wake huyo aliambukizwa ugonjwa wa zinaa.

Mtoto huyo wa mtuhumiwa na mdogo wake wa kiume walichukuliwa na kwenda kulelewa na watu maalum wakati kesi ilipoanza kuunguruma.

Wakiwa huko, Juni 29, mwaka huu, mama anayemlea alimsikia binti huyo, wakati anamvua nepi, akimlalamikia mwanamme ambaye mlezi huyo hakumjua.

“Baba inaumiza.  Baba, usiwe katili.  Baba, inaumiza,” alikuwa akilalamika mtoto huyo.

Polisi wamemkata mwanamme mmoja Charles Green (43) kwa mashitaka mawili ya kuhatarisha maisha ya mtoto.  Mtu huyo anadaiwa kuwa mpenzi wa Watson.

Mtuhumiwa Charles Green.

Hati za mahakama zinasema Green na Watson walipanga ukatili huo licha ya Watson kudai huwa anamwogopa Green.

Polisi wamesema hawajampata mtuhumiwa yeyote, na watoto wanaendelea kuwa chini ya ulezi wa watu wengine.

Comments are closed.