The House of Favourite Newspapers

Sakata la Lugumi, NIDA: Lugola Ampa Mtihani Sirro – Video

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro ametakiwa kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya Lugumi popote pale alipo na kumfikisha ofisini kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola,  ifikapo Julai 31 mwaka huu, saa 2:00 asubuhi.
Amri hiyo imetolewa na Waziri Lugola alipozungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali ya wizara yake ambapo pia alimuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) afike ofisini kwake Julai 25 akiwa na watu waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya taifa ambao bado haujaletwa licha ya kupewa pesa husika.
Akirejea sakata la kampuni ya Lugumi  alisema mkataba uliofikiwa kati ya wizara yake na kampuni hiyo ambapo ilipewa kazi ya kununua na kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole, haijakamilika.
“Hao ambao waliopita (mawaziri Charles Kitwanga na Mwigulu Nchemba) hawakuwa ‘maninja’, sasa amekuja ‘Ninja’ anamtaka Lugumi aje,” alionya waziri huyo.
Na Edwin Lindege | Global Publishers

MSIKIE LUGOLA AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.