The House of Favourite Newspapers

MAMA AMTIMUA BWANA WA WEMA USIKU MNENE

IMEVUJA! Mama mzazi wa mwigizaji wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu anadaiwa kumfanyia varangati la kufa mtu mwanaume aliyekuwa na uhusiano na bintiye anayefahamika kwa jina moja la R.a.h.u.r, Ijumaa Wikienda limenasa tukio zima.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo ‘uwanja wa mapambano’ inaelezwa kuwa ilikuwa ni nyumbani kwa Wema, maeneo ya Mbezi-Salasala jijini Dar.

 

CHANZO CHASHUSHA DATA

Awali, Ijumaa Wikienda lilipewa mchapo kuwa, mama Wema ambaye hakuwa akifurahishwa sana na uhusiano wa bintiye na ‘mkwewe’ huyo, aliibuka nyumbani hapo kwa mwanaye na kumtolea uvivu baada ya kuona jamaa si mtu wa maana.

Chanzo: Hapo si ni Ijumaa Wikienda?

Ijumaa Wikienda: Ndiyo hujakosea, leta habari!

Chanzo: Mna ubuyu wa mama Wema?

Ijumaa Wikienda: Tunao mwingi tu ambao umeshakamilika, mwingine bado tunaendelea kuufuatilia, wewe una upi?

Chanzo: Mimi ninao wa kumtimua bwana wa Wema pale nyumbani kwa Wema, Salasala…

Ijumaa Wikenda: Huo tuliusikia mahali, lakini kuna ‘doti’ zilikuwa hazijakamilika, hebu simulia kwanza tukusikie wewe.

AUSHUSHA UBUYU KAMA WOTE

“Iko hivi, mama Wema siku nyingi tu alikuwa akimsikiasikia huyo bwana, sasa siku hiyo ndiyo akamkuta nyumbani kwa Wema.

“Na kwa bahati mbaya siku hiyo alipokuja, alimkuta, yeye akawa bize na mambo yake, Wema hakuwepo.

“Ilipofika usiku, luku ilikata umeme, mama Wema akasubiri kwa muda, hakuna aliyekuwa tayari kununua.

 

AKINUKISHA

“Baada ya kuona muda unaenda na yule bwana wa Wema hana dalili za kununua umeme, ndipo alipoamua kukinukisha kwa kumchana kuwa hataki kumuona katika nyumba hiyo.

“Jamaa alitaka kuleta kipingamizi kiaina, lakini kama unavyojua mziki wa mama Wema si wa nchi hii, mwenyewe alilainika na kuamua kushika njia huku akiwa ameinamisha kichwa kwa aibu,” kiliweka nukta chanzo hicho makini.

 

JAMAA AMEONDOKA MAZIMA?

Chanzo hicho kilieleza kuwa, tangu siku hiyo, jamaa huyo hakuwahi kuonekana tena nyumbani hapo kwa Wema na sasa wanaonekana mara kwa mara nyumbani hapo ni baadhi ya wasaidizi wake wa karibu Wema akiwemo dada wa kazi.

“Haonekani siku hizi, nahisi ameona nishai kile kitendo cha yeye kuondolewa kwa maneno makali akaamua asepe jumla,” kilisema chanzo hicho.

 

MAMA WEMA ANASEMAJE?

Baada ya kuupata ubuyu huo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya mama Wema ambapo alipopatikana alianza kwa kusema kuwa, hamtambui mwanaume huyo na ndiyo maana alimtimua.

“Hakuna mwanaume yeyote ambaye Wema amenitambulisha hivyo ndiyo maana nilimtimua. Naona na kuyasikia haya mambo kwenu waandishi, lakini hakuna mtu ambaye mimi namfahamu yupo na mwanangu,” alisema mama Wema.

Alipoulizwa kama sababu iliyomfanya amtimue bwana huyo ni luku tu au kuna nyingine iliyokuwa nyuma ya pazia, mama Wema hakuwa tayari kuzungumzia zaidi ya kusema kuwa hamtambui mwanaume yeyote ambaye yupo na binti yake kwa sasa.

Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa, Wema na jamaa huyo kwa sasa wameshamwagana na ana mtu mwingine ambaye bado hajamuweka wazi, achilia mbali kuingia kwenye kumi na nane za Ijumaa Wikienda.

 

HUYU HAPA R.A.H.U.R

Baada ya kumalizana na mama Wema, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya R.a.h.u.r ambapo alipopatikana alidai kuwa madai yaliyoelezwa si sahihi kwani yamepindishwa.

“Si kweli kwamba mimi nimegombana na huyo mama kwa sababu eti ya luku, mimi nashindwa kununua luku ukiniangalia? Huyo mama hakutaka niwe karibu na mwanaye kwa madai sijui hayuko vizuri anaumwa,” alisema R.a.h.u.r.

WEMA VIPI?

Jitihada za kumsaka Wema ili kumsikia anamzungumziaje sakata hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa. Jitihada zinaendelea!

 

TUJIKUMBUSHE

Kwa muda mrefu Wema amekuwa kimya kumuanika mpenzi wake tangu alipofanya hivyo mara kadhaa kwa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye awali walijianika hadharani, wakamwagana na baadaye wakarudiana kisha wakamwagana jumla.

Hata hivyo, Magazeti ya Global Publishers kwa nyakati tofauti yalifichua bwana’ke mmoja ambaye baadaye alipata msala wa madawa ya kulevya nchini Kenya ambaye kesi yake bado inaunguruma.

Comments are closed.