The House of Favourite Newspapers

Mama Janeth Maguful Atunukiwa Tuzo Ya Kimataifa, Mchango Wake Kwa Hayati Magufuli

0

Mama Janeth Magufuli, mke wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli akionesha tuzo hiyo.
Mama Janeth Magufuli, mke wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo
Mama Janeth Magufuli, mke wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametunukiwa Tuzo ya Heshima nchini DRC kwa mchango wake alioutoa kwa mwenza wake alipokuwa madarakani.
Tuzo za M. T. KASALU zinatolewa na Taasisi ya LIZADEEL kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi ya DRC, UNESCO, UN-WOMEN na Asasi za Kiraia. Mama Janeth Magufuli ni miongoni mwa Washindi sita wa Toleo la Tatu la Tuzo hizo zilizokuwa zinawaniwa na wanawake 150.
Washindi wengine ni kutoka Nchi za DRC (2), Senegal, Ufaransa na Marekani.
Leave A Reply