Mama, Mimi Ndio Injini ya Mobeto

MAMA mzazi wa mwanamuziki Hamisa Mobeto, Shufaa Lutiginga amefunguka kuwa yeye ndiyo injini ya kila anachokifanya mwanaye.

 

Mama Hamisa ambaye Jumanne iliyopita aliambatana na mtoto wake huyo kwenye Usiku wa Tamasha la Bonsi Vibe Festival lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, alisema yeye ndiyo huipangia ‘management’ ya mwanaye kila kitu.

 

“Watu watarajie shoo kali zaidi ya hii ndani na nje ya nchi naongea hivyo kwa sababu mimi ndiyo injini ya Mobeto, mimi ndiye msimamizi mkuu wa kila jambo kwa maana hata management yake mimi ndiye ninayetoa madaraka hivyo hakuna kinachoweza kuharibika, watu wakae mkao wa kula,” alisema mama Hamisa.


Loading...

Toa comment