MAMA MONDI AFUNGUKIA MADAI YA NDOA YAKE KUVUNJIKA

MAMBO ni motrooo! Siku chache baada ya tetesi kusambaa mitandaoni kuwa ndoa yake na mumewe, Maisala Shamte ‘Anko’ imevunjika, mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ Sanura Kassim ‘Bi Sandrah’ amefunguka. 

 

Awali habari zilizolifikia gazeti hili licha ya mitandao kuchafuka, baada ya kusambaa taarifa kuwa mama huyo ambaye ni kiboko kwa ‘vijembe’ mitandaoni ameamua kujitenga mbali na Shamte.

 

“Kwa sasa mama Mondi siyo yule mnayemjua, amekuwa mdogo kama piritoni, jamaa (Shamte) ameshamnyoosha huko mitandaoni ni furaha tu,” kilidokeza chanzo hicho na kuongeza;

“Ujue ipo hivi, wakati Shamte mapenzi yamemkolea kwa mama Mondi kumbe nyuma yake yupo katika uhusiano na mwanamke mwingine mbaya zaidi amezaa naye na kumpangishia nyumba kwa siri. Sasa hivi pamewaka moto mama Mondi ameshajua ukweli na hawapatani tena,” kiliweka nukta chanzo hicho.

Risasi Mchanganyiko pia lilichungulia katika mitandao ya kijamii ambayo nayo ilikuwa imechafuka vya kutosha juu ya ndoa ya mama Mondi na Shamte kuvunjika;

“Mimi nilijua tu Shamte hawezi kuendelea kuwa na yule bi Sandra, yaani yule kaka alifuata pesa tu pale hakuna kitu kingine, sasa ameshazipata kaenda kuzaa na mtu mwingine,” aliweka komenti @ Ivvydaud mmoja wa mashabiki katika mtandao wa Instagram.

 

Gazeti hili lilimvutia waya Shamte kwa lengo la kutaka kujua kama hizo tetesi zinazosambaa ni za kweli au la, ambapo baada ya kupigiwa mara mbili simu ilipokelewa na kisha muhusika kukaa kimya bila kuongea kitu. Alipotafutwa kwa mara ya tatu ndipo akapokea mama Mondi kwa kupitia simu ya Shamte na kufungukia kuvunjika ndoa yake hiyo;

 

Risasi Mchanganyiko: Hallo!

Mama Mondi: Hallo, nakusikiliza mimi mama Nasibu naongea.

Risasi Mchanganyiko: (Kwa kushtuka kidogo maana hakutegemea kama simu ingepokelewa na mama Mondi) Ahaa heshima yako mama, nilikuwa nampigia Shamte ili nipate uhakika wa kile kinachozungumzwa mitandaoni kuwa mmeachana baada ya yeye kumzalisha mwanamke mwingine nje na kumpangia nyumba.

Mama Mondi: Ndio mimi mama Nasibu nishapokea sasa, ongea!

Risasi Mchanganyiko: Eeeh mama hizo tetesi ni za kweli?

Mama Mondi: Hivi ingekuwa kweli mimi ningepokea simu yake asubuhi yote hii? Sisi hatuwezi kuachana kwa mambo yasiyo kuwa na maana, tunapendana asikuambie mtu sasa waache wanafki waendelee kusambaza mambo ya umbea huko mitandaoni huku sisi yetu yanatunyookea.

 

Ikumbukwe kwamba Bi Sandrah anadaiwa kufunga ndoa ya siri na Shamte ambayo ilihudhuriwa na watu wachache na maalumu, pia katika mahojiano mara kwa mara amekuwa akikiri kufunga ndoa hiyo. Kabla ya kuwa na Shamte, Bi Sandra alishawahi kuwa na uhusiano na baba Diamond, Abdul Juma.

Loading...

Toa comment