The House of Favourite Newspapers

MAMA MWENYE NYUMBA AMNYOOSHA GIGY MONEY

Gift Stanford ‘Gigy Money’

DAR ES SALAAM: Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuhamia kwenye nyumba mpya aliyopanga maeneo ya Kijitonyama, jijini Dar, mama mwenye nyumba wake anayejulikana kwa jina la Mama Koku anadaiwa kumnyoosha mwanadada huyo kwa kumpa masharti magumu.  

 

Habari zilieleza kuwa Gigy alipewa masharti hayo magumu na mama huyo ambaye alikuwa anaijua historia ya msanii huyo kwani alikotokea aliwahi kugombana na mwenye nyumba mpaka kutaka kumshushia kipigo.

 

“Yaani Gigy alipoingia tu kwenye hii nyumba alipewa masharti makali kama vile kutovaa nguo za ajabu, kulewa, kuvuta bangi na kubadili wanaume hivyo akiwa anatoka kama amevaa nguo za nusu utupu anafunga kanga anaenda kuvua nje,” alisema mmoja wa majirani wa Gigy.

 

Risasi Mchanganyiko baada ya kupata habari hizo lilianza kazi ya kutafuta anakoishi Gigy na kufanikiwa kupapata ambapo hakuwepo nyumbani hivyo walizungumza na mwenye nyumba wake ambaye alifunguka maisha ya msanii huyo.

 

“Ni kweli Gigy anaishi hapa na kwa sasa ametoka na mwanaye Mayra, waliopo ni dada wa kazi na mdogo wake, kiukweli Gigy alipohamia tu kwangu hapa nilimpa masharti kwa sababu nilishasikia habari zake huko alikotoka.

 

“Kutokana na sifa zake hizo nilimwambia ni marufuku kuvaa nusu utupu, kubadili wanaume kila kukicha kama anaye mmoja awe ndiye huyohuyo, kweli amekuwa akifuata masharti hayo na tunaishi vizuri tu.”

 

MADAI YA KUGEUZA CHUMBA DANGURO

Mama huyo alipoulizwa kuhusiana na Gigy kudaiwa kugeuza chumba chake danguro ambapo wanaishi wanawake watatu na wanaume watatu huku wakilewa na kuvuta bangi mama huyo alisema si kweli.

 

“Kiukweli huyu binti humu ndani wanaishi wanne tu, yeye, mdogo wake, mtoto pamoja na dada wa kazi, hao watu mnaowasema hawaishi hapa ni watu ambao huwa wanakuja tu na kuondoka, kama mnavyojua huyu mtu ni staa kwa hiyo lazima atembelewe na watu wengi.

 

“Lakini nakumbuka alivyokuwa anataka kuhamia hapa, nilikaa naye na nikampa masharti yangu, kwa sababu nilisikia huko alikokuwa anaishi aligombana na mwenye nyumba wake.

 

“Sasa nilimwambia kwamba kama anataka kuishi vizuri na mimi hapa nyumbani kwangu sihitaji matusi na nilimpiga marufuku kuvaa vinguo vifupi hapa nyumbani kwa sababu nina watoto wadogo kwa hiyo sitaki waige tabia mbaya, nikamweleza kama anahitaji kuvaa nguo fupi awe anavaa akishatoka nje ya geti lakini siyo humu ndani.

 

“Kuhusu kuvuta sigara na kutumia siwezi nikamzuia mtu kufanya kitu anachokipenda, pengine hiyo ndiyo furaha yake mimi nitajuaje, ila nashukuru Mungu kwa sababu naishi vizuri tu na huyu binti na ni mtafutaji sana, nampongeza kwa hilo.”

 

Alipoulizwa kuhusu baba mtoto wa Gigy yaani Mo J kama anaishi naye hapo mama huyo alimalizia kwa kusema; “Sijawahi kumuona baba wa huyo mtoto tangu ahamie ila najua ana uhusiano na kijana mmoja Mmarekani na anaishi Nairobi, alishakuja hapa akakaa siku tatu na Gigy huwa anaenda na hata siku za hivi karibuni alikuwa huko.”

Stori:NEEMA ADRIAN NA MEMORICE RICHARD, RISASI MCHANGANYIKO

LAVALAVA: “Diamond Ana Mapungufu / Tunavumilia / Alikiba…”

Comments are closed.