The House of Favourite Newspapers

MAMA SAMIA AZINDUA KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA

Mhe. Samia Suluhu Hassan.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuzinduka Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’, amemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aunde kamati itakayozunguka Tanzania nzima kuhamasisha uzalendo.

Mama Samia, amesema hayo jana mkoani Dodoma wakati akizindua rasmi Kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’, ambapo alimuomba Waziri Mwakyembe kuunda kamati ndogo itakayozungumza nchi nzima kuhamasisha Watanzania kuwa na uzalendo wa kweli wa nchi yao.

 

“Nikuombe Waziri Mwakyembe kuunda kamati ndogo kwa ajili ya kuzunguka maeneo yote ya nchi yetu kuhamasisha uzalendo na utaifa. Uzalendo siyo kipaji bali unajengwa na kuandaliwa na jamii husika, kampeni hii inatoa fursa ya kuelimisha vijana umuhimu wa Tamaduni, Sanaa, Mila na Maadili ya Kitanzania. Tufanye mambo kwa wakati, wakati tuna wakati ,tuutumie wakati vizuri kutekeleza mambo yetu,” alisema Makamu wa Rais, Mama Samia.

 

Kwa upande wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuwa wazalendo kwa kupenda mila na tamaduni zao, kwa sababu huizo ndizo alama zinazoitambulisha na  kuitofautisha Tanzania na mataifa mengine.

 

“Tuwe wazalendo kwa kupenda sanaa na tamaduni zetu zinazotutambulisha sisi kama Watanzania, ufanye kazi kwa bidii ili tuzalishe mali kwa wingi na kujenga taifa letu, huo ndiyo uzalendo.

 

“Tunayo sababu ya kumuunga mkono Mhe.Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwahamasisha Watanzania kuwa wazalendo, suala hili si geni hivyo ni wajibu wetu kuudumisha kwa maslahi ya taifa letu na ili kufikia uchumi wa viwanda ni wajibu wetu kuwa wazalendo kwa kusimamia rasilimali zetu,” aliongeza Majaliwa.

 

Naye Waziri wa Habari Dkt Mwakyembe alisema kuwa, kufikia mwaka 2063 Lugha ya Kiswahili itakuwa lugha kuu barani Afrika na utambulisho wa mtu mweusi. Watanzania tuipokee kampeni hii kwa mikono miwili kwa kuwa ni kampeni ambayo inaenda kulifanya taifa la watu ambao wako tayari kufa kwa ajili ya nchi yao.

 

Kampeni hiyo iliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Taasisi ya Mpoto Theatre Gallary ina nia ya kuwakumbushwa Watanzania, suala la uzalendo ikiwemo kuepuka rushwa, kuvunja miiko na maadili ya viongozi kwa Umma na kufufua uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

Baadhi ya wasanii walioshiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo na kuimba wimbo maalumu ni Mrisho Mpoto, Fid Q, Ray C, Witness Mwaijaga ‘Kibonge Mwepesi’, Kassim Mganga na wengineo.

 

JPM KAAGIZA! Babu Seya, Papii Kocha, Waachiwe Huru!

Comments are closed.