The House of Favourite Newspapers

Mama Samia: Taifa Limepoteza Mtu Muhimu – Video

0

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassam, amesema kwamba kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kimelifanya taifa kupoteza mtu muhimu,

 

Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020, alipofika nyumbani kwa Mkapa, Masaki jijini Dar es Salaam kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki.

 

“Kama kuna jambo kubwa la nchi, akisimama Mkapa basi tunajua suluhu itapatikana. Afrika imepata mshtukoo. Hiyo ni kazi ya Mungu, hatuna budi kuipokea.

“Tumepoteza mtu muhimu na sasa kinachofuata baada ya kifo chake ni kufuata fikra zake, mienendo na miongozo yake katika kuiongoza nchi hii,” amesema.

 

Mkapa alifariki dunia usiku wa kuamkia jana Ijumaa  Julai 24, 2020 na mwili wake, utazikwa Jumatano  Julai  29, 2020, kijijini kwake Lupaso Mkoa wa Mtwara.

Leave A Reply