The House of Favourite Newspapers

MAMBO 5 USIYOYAJUA KUHUSU TANASHA

NI mwa-nam-ke pekee aliyenionesha yupo makini na ana sifa zote za kuingia naye kwenye ndoa na sasa ni rasmi ninatangaza kwamba ninamuoa…

“Ana sifa zote ambazo mwanaume yeyote aliyekamilika angetamani awe mkewe. Sisi wanaume tulio wengi huwa tunaangalia shepu, maumbile, mvuto wa nje na mengineyo ambayo yote anayo. Lakini kikubwa zaidi kuliko vyote ni TABIA! Ana tabia nzuri.”

 

Haya ni maneno ya mwanamuziki anayepeperusha bendera ya Bongo Fleva barani Afrika na kwingineko duniani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Ilikuwa Novemba 23, mwaka jana alipokuwa akithibitisha kuwa kwenye uhusiano rasmi wa kimapenzi na mrembo kutoka nchi jirani ya Kenya, Tanasha Donna Oketch. Ulikuwa msimu wa lile Tamasha la Wasafi lililo chini ya Diamond.

 

Kauli hiyo ilishtua mashabiki wengi wa Diamond au Mondi. Kila mmoja alitaka kumjua ni nani huyo mwenye ubavu wa kurithi nafasi ya Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mwanamke aliyemzalia jamaa huyo watoto wawili, jike na dume, Tiffah Dangote na Prince Nillan. Mwanamama tajiri kutoka Uganda, anayejituma kutafuta pesa na aliyeaminika ana sifa zote za mke na mama bora! Shauku hiyo inaifanya ShowBiz Extra kuchimba na kuibuka na mambo matano (5) yanayo-mhusu Tanasha juu ya yeye ni nani hasa?

 

1: MISS WORLD KENYA

“Naitwa Tanasha Donna Barbieri Oketch a.k.a Zahara Zaire. Nina umri wa miaka 22 (mwaka 2018). Mimi ni chotara. Mchanganyiko wa Mkenya na Muitaliano. Nimekulia Kenya. Niliondoka Kenya nikiwa na umri wa miaka 11 na kwenda Ulaya. Nikiwa Ulaya, nilianza kujihusisha na mitindo tangu nikiwa na umri mdogo. Nilishiriki maonesho mbalimbali likiwemo Miss Afrika-Ubeligiji. Baadaye nilirejea nyumbani Kenya, nilitaka kushiriki Shindano la Miss World- Kenya. Niliposhindwa ndiyo nikaweka makazi hapa nyumbani Kenya.

2: ELIMU

“Kuhusu elimu, baada ya shule za awali nilisoma masuala ya utalii nchini Ubeligiji. Nilijifunza lugha mbalimbali za kigeni. Ninaweza kuzungumza na kuandika lugha tano za Kingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kidachi na Kihispaniola.

3: FANI

“Kwa sasa mimi ni mtangazaji wa redio (NGR ya Mombasa, Kenya). Ni video vixen (video queen ambaye aliuza sura kwenye Video ya Nagharamia ya Alikiba na Christian Bella).

4: HARAKATI ZA KUTOKA

KIMAISHA

“Mimi ni mjasiriamali, nimewekeza kwenye bidhaa za urembo, ndiye mkurugenzi na mmiliki wa Kampuni ya For Her Luxury Hair inayosambaza bidhaa ya nywele.

5: UHUSIANO

“Ni kweli niliingia kwenye uhusiano wa Nick Mutuma (Mwigizaji wa kiume wa Kenya). Ulidumu kwa miezi saba tu kabla ya kuvunjika Agosti, 2017. Of course kwa sasa ni mpenzi wa Diamond Platnumz,” alikariri Tanasha na Jarida la Tag la nchini Kenya.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.