The House of Favourite Newspapers

MAMBO MUHIMU 20 YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA

 

Safari ndefu katika maisha ya mwanadamu huwa yanakuwa na furaha pale linapofikia swala na ndoa na kuwa na familia kwasababu hili ndilo jambo muhimu lililotuleta duniani.

 

Lakini endapo utakosea kwenye ndoa basi unawezekana ukawa umeharibu furaha nzima ya maisha yako kwani familia nzuri pendwa na yenye amani hujengwa na ndoa yenye furaha.

 

Hakikisha unapata elimu maalumu nay a kutosha kabala ya kuingia kwenye stage/hatua kubwa ya ndoa wewe na mwenza wako kwa pamoja lakini hata kama mmeshaoana na hamkupata elimu hiyo, hamjachelewa inawabidi mpate elimu mapema ili kuifanya ndoa yenu kuwa salama na yenye nguvu.

 

Mambo haya 20 sio kwa asilimia 100, nikimaanisha sio kwa wote wana tabia hizi, ili ni uchunguzi mdogo uliofanywa na ukaonyesha asilimia kubwa sana ya watu au mambo yapo hivyo.

 

Yajue na kuwa makini na mambo haya kabla ya kuingia kwenye ndoa.

1.Sherehe ya Harusi ni ya siku moja tu, na Ndoa
ni ya maisha yote.

 

2.Mwanamume/Mwanamke aliyezoea kuchepuka
kabla ya Ndoa, ataendelea kuchepuka hata baada
ya Ndoa.

3.Upole na ukimya si kiashiria cha tabia njema.

 

4.Ukikitaka ambacho hakijawahi milikiwa na mtu
yeyote, ni lazima ufanye jambo ambalo halijawahi
fanywa na mtu yeyote

5.Mungu akitaka kukubariki hukuletea mtu, na
Shetani akitaka kukuangamiza hukuletea mtu.

 

6.Bora uishi mwenyewe kuliko kuoa ama
kuolewa na mtu hasiye sahihi.

 

7.Aina tatu za wanaume wakuepukwa:
a) Walevi. b) Malaya. c)Wagomvi.

8 .Kuolewa na Mchekeshaji hakutakufanya uwe
na Ndoa yenye furaha

 

9.Maneno matatu yanayojenga amani katika
Ndoa:
a) Nakupenda. b) Samahani. c) Asante.

 

10.Kupiga punyeto ni kujiharibu.

 

11.Kuoana kabla ya kuwa marafiki ni kama anga
bila jua.

 

12.Mafanikio ya Ndoa siku zote ni pembetatu:
Mungu mmoja – Mume mmoja – Mke mmoja.

 

13.Furaha ya kudumu maisha hutegemea na
chaguo lako la Ndoa.

 

14.Usioe pesa au mali – muoe mtu.

 

15.Uchumba uliovunjika ni bora zaidi kuliko Ndoa
isiyo na amani na furaha.

 

16.Usiweke kipaumbele chako kwa muonekano
mzuri wa mwanamke. Hakuna mwanamke
mbaya, bali anahitaji kupendezeshwa.

 

17.Mapenzi si upofu. Upofu ni kuoa ama
kuolewa na mwanamume/mwanamke kwa kigezo
tu anakidhi haja zako kingono.

 

18.Ukiwa rafiki mwema, utawavutia marafiki
wema.

 

19.Asili ya mikono inayojali ni moyo unaojali.

 

20.Iepuke Ndoa mbaya kabla haijaanza…

Comments are closed.