The House of Favourite Newspapers

SIMBA WAMWONDOA UDHAMINI, WAMSIMAMISHA UANACHAMA KILOMONI

0
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe,  akiongea na wanachama wakati wa mkutano.
Msemaji wa Simba, Haji Manara, akiongea na wanachama.
Wanachama wa klabu ya Simba wakiwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Wanachama wa klabu ya Simba wakipitisha hoja kwa pamoja ya kuondolewa kwenye udhamini, Mzee Hamisi Kilomoni.
Kamati Kuu ya uongozi wa Simba wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kwa kikao
Katibu Mkuu wa Simba, Alex Kashembe (kulia), akiongea jambo na Hans Poppe.
Zacharia Hans Poppe akitafakari jambo.
Wanachama wakipata chakula baada ya mkutano.

 

KLABU ya Simba  leo wamefanya Mkutano Mkuu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza mikutano ya aina hiyo ya klabu hiyo kufanyika katika ukumbi wa kisasa.

Wanachama waliofika kwenye mkutano huo ni zaidi ya 500 kati ya 927 waliojiandikisha ambapo wamepitisha azimio la kumuondoa akwenye udhamini, Mzee Hamisi Kilomoni  na kumsimamishwa uanachama  na wamesema kwamba asipofuta kesi mahamakani na kuomba radhi, atafutwa kabisa uanachama.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Adam Mgoyi, ameteuliwa kuwa mdhamini mpya wa klabu kuchukua nafasi ya Mzee Kilomoni kwenye baraza la wadhamini.

Mkutano huo pia umemthibitisha Juma Othuman Kapuya kuwa mdhamini wa klabu kuziba pengo la mzee Ally Sykes aliyefariki dunia.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema:  “Bado tunawatambua viongozi wetu wakuu,  Rais Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange kwa kuwa bado hawajakutwa na hatia.  Mali za klabu ni mali za wanachama na si za Mzee Kilomoni kwa mujibu wa katiba ya Simba.  Simba ikifanikiwa kuingia kwenye mfumo wa uendeshwaji kwa hisa itakuwa klabu namba mbili Afrika kwa thamani.

“Nampongeza pia Rais wa TFF, Karia, Makamu wake Wambura na Kamati nzima ya Utendaji, tunawatakia kila la heri katika  majukumu yao mapya.”

(PICHA:  GLOBAL TV ONLINE)

Leave A Reply