The House of Favourite Newspapers

Mambosasa Asema Miili Iliyokutwa Kwenye Viroba Hajui Ilikotoka

0
Lazaro Mambosasa.

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema miili ya wanaume watatu iliyokutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach hawajui imetoka wapi hivyo wanaendelea na uchunguzi kubaini ilipotoka.

Mambosasa amesema jeshi la polisi linaendelea kupeleleza ili kujua miili hiyo imetokea mkoa upi, nchi gani na wajulikane watu hao ni wakina nani.

“Miili hiyo haieleweki inatoka wapi na watu wenyewe hawajulikani kama wanatoka Tanzania, Msumbiji au Angola hivyo tunaendelea kuichunguza,” amesema Mambosasa.

Maiti za watu ziliokotwa juzi katika eneo hilo mbili zilifungwa kwenye viroba huku nyingine imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.

Kubenea Aitaka Serikali Kulifungulia MwanaHalisi Ndani ya Siku 2

Leave A Reply