The House of Favourite Newspapers

Mambosasa: Uchaguzi wa leo tutawadhibiti wahalifu

Kamanda wa polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

 

 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa jeshi lake limeimarisha ulinzi wa kutosha kila eneo ili kuhakikisha hakuna vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani vitakavyotokea.

 

Akizungumza na wanahabari, Mambosasa amesema  kuwepo askari wengi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni ni dalali njema za kuwepo kwa amani na utulivu hivyo wananchi wasihofie kuwepo kwa vurugu yoyote na uchaguzi utaisha salama.

 

“Askari wapo Stand by kutoka eneo lolote la wilaya za Dar es Salaam pale watakapohitajika kuongeza nguvu katika Wilaya ya Kinondoni,” alisema.

 

Akaongeza kuwa usalama wa raia upo vizuri na hakuna vurugu yoyote iliyotokea kuanzia asubuhi hadi majira ya saa kumi, lakini ametoa onyo kwa tetesi ambazo amesikia kwamba kuna makundi ya watu wanaotarajiwa kutokea maeneo ya Ilala la Temeke kuelekea Kinondoni kwa ajili ya kujikusanya na kufanya uhalifu, hivyo jeshi lake halitamvumilia mharifu.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

VIdeo: Msikie hapa akizungumza.

Comments are closed.